Mark 13

1Yesu alipokuwa akitembea kutoka hekaluni, mmoja wa wanafunzi wake akamwuliza, “Mwalimu, tazama mawe haya yakushangaza na majengo!” 2Akamwambia, Unaona majengo haya makubwa? Hakuna hata jiwe moja litakalo salia juu ya jingine ambalo halitaangushwa chini”.

3Naye alipokuwa amekaa juu ya Mlima wa Mizeituni nyuma ya hekalu, Petro, Yakobo, Yohana na Andrea wakamwuliza kwa siri, 4“Tuambie, mambo haya yatakuwa lini? Ni nini dalili ya mambo haya kutokea?”

5Yesu alianza kuwaambia, “Kuweni makini kwamba mtu yoyote asiwapotoshe. 6Wengi watakuja kwa jina langu wakisema, ‘Mimi ndiye’, na watawapotosha wengi.

7Mtakaposikia vita na tetesi za vita, msiogope; mambo haya hayana budi kutokea, lakini mwisho bado. 8Taifa litainuka kinyume na taifa jingine, na ufalme kinyume na ufalme. Patakuwa na matetemeko sehemu mbalimbali, na njaa. Huu ni mwanzo wa utungu.

9Iweni macho. Watawapeleka hadi mabarazani, na mtapingwa katika masinagogi. Mtasimamishwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, kama ushuhuda kwao. 10Lakini injili lazima kwanza ihubiriwe kwa mataifa yote.

11Watakapo wakamata na kuwakabidhi, msiogope kuhusu kile mtakachosema. Ndani ya muda huo, mtapewa nini cha kusema; hamtakuwa ninyi mtakaoongea, bali Roho Mtakatifu. 12Ndugu atamshitaki ndugu kuuawa, baba na mtoto wake. Watoto watasimama kinyume cha baba zao na kuwasababisha kuuawa. 13Mtachukiwa na kila mtu kwa sababu ya jina langu. Lakini atakayevumilia mpaka mwisho, mtu huyo ataokoka.

14Mtakapoona chukizo la uharibifu limesimama pale lisipotakiwa kusimama (asomaye na afahamu), ndipo walioko ndani ya Yuda wakimbilie milimani, 15naye aliyeko juu ya nyumba asishuke chini ya nyumba, au kuchukua chochote kilichoko nje, 16na aliyeko shambani asirudi kuchukua vazi lake.

17Lakini ole wao wanawake wenye mimba na wanyonyeshao katika siku hizo! 18Ombeni kwamba isitokee wakati wa baridi. 19Kwani patakuwa na mateso makubwa, ambayo hayajawahi kutokea, tangu Mungu alipoumba ulimwengu, mpaka sasa, hapana, wala haitatokea tena. 20Mpaka Bwana atakapopunguza siku, hakuna mwili utakaookoka, lakini kwa ajili ya wateule, atakaowachagua, atapunguza namba za siku.

21Wakati huo kama mtu yeyote atawaambia, Tazama, Kristo yuko hapa!’ au ‘Tazama, yuko pale!’ msiamini. 22Kwani Wakristo wa uongo na manabii wa uongo watatokea na watatoa ishara na maajabu, ili kwamba, wawadanganye, yamkini hata wateule. 23Iweni macho! Nimekwisha wambia haya yote kabla ya wakati.

24Lakini baada ya mateso ya siku hizo, jua litatiwa giza, mwezi hautatoa mwanga wake, 25nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu zilizoko mbinguni zitatikisika. 26Ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni kwa nguvu kubwa na utukufu. 27Ndipo atatuma malaika zake na atawakusanya pamoja wateule wake kutoka pande kuu nne za dunia, kutoka mwisho wa dunia mpaka mwisho wa mbingu.

28Kwa mtini jifunzeni. Kama tawi liwezavyo kutoa na kuweka haraka majani yake, ndipo mtajua kwamba kiangazi kiko karibu. 29Ndivyo ilivyo, mtakapoona mambo haya yakitokea, jueni kwamba yuko karibu, na malango.

30Kweli, nawambieni, hiki kizazi hakitapita mbali kabla mambo haya hayajatokea. 31Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe. 32Lakini kuhusu siku hiyo au saa, hakuna ajuaye, hata malaika wa mbinguni, wala Mwana, ila Baba.

33Iweni macho, Tazama, kwa sababu hamjui ni muda gani yatatokea. (Zingatia: Mstari huu, “Muwe waangalifu, Tazameni na ombeni kwa sababu...” haumo kwenye nakala za kale). 34Ni kama mtu anayeenda safarini: akaacha nyumba yake, na kumweka mtumwa wake kuwa mtawala wa nyumba, kila mmoja na kazi yake. Na kumwamuru mlinzi kukaa macho.

35Kwa hiyo iweni macho! Kwani hamjui ni lini bwana wa nyumba atakaporudi nyumbani, yawezekana ni jioni, usiku wa manane, wakati jogoo atakapowika, au asubuhi. 36Kama akija ghafla, asikukute umelala. Kile nikisemacho kwako nakisema kwa kila mtu: Kesheni”!

37

Copyright information for SwaULB